.

.

.

.

Friday, January 30, 2009

MH.MIZENGO PINDA ATOA MACHOZI BUNGENI


Waziri Mkuu alifikia hali hiyo wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Hamad Rashid Mohamed, aliyemtaka aeleze sababu zilizomfanya atoe kauli ya watu wanaowaua maalbino nao pia wauawe. Pinda alitoa kauli hiyo hivi karibuni akiwa ziarani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Juzi, kambi hiyo ilitoa tamko mbele ya waandishi wa habari ikimtaka Waziri Mkuu aachie ngazi kutokana na kauli hiyo kwa madai kwamba inapingana na utawala bora wa kisheria. Baada ya kupewa nafasi na Spika, Samuel Sitta, kuuliza swali la nyongeza, Kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni alipomuuliza swali lililomfanya Waziri Mkuu ashindwe kuvumilia kutoa machozi wakati akielezea adha wanazozipata maalbino. ``Kwa mtu ambaye hajapata nafasi ya kukutana nao (maalbino) na wakamueleza wanayoyapata…(sauti yake ikabadilika ghafla na kutokwa na machozi), wauaji hawa hawawezi kuvumiliwa. Katika mazingira kama haya, Watanzania hatutakuwa tayari kuwavumilia wauaji hao,`` alisema kwa sauti ya huruma.
Picha na habari kwa Hisani ya IPPMEDIA

No comments:

Post a Comment