.

.

.

.

Tuesday, January 06, 2009

MOHAMED ABDUL SHAKUR ATUTOKA ITALY

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Italy unasikitika kutangaza kifo cha Ndugu MOHAMED ABDUL SHAKUR (PAMA) kilichotokea jana asubuhi katika hospitali ya SAN GIOVANNI DI DIO E RUGGI D'ARAGONA" SALERNO.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy,kwa niaba ya uongozi na watanzania wote hapa Italy,anapenda kutoa salam za rambirambi kwa wazazi na ndugu wa marehemu nyumbani na popote walipo,kuwa tumepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa na tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu wa maombolezo.Mungu ailaze roho yake mahala pema . Amin.

KWA WALE WOTE WALIO NJE YA ITALY KWA MAWASILIANO TUPIGIGIE SIMU NAMBA: +39 3271753565(Mwenyekiti) AU +39 3453118431 (DULLAH) au +39 331 8360509 (Katibu mkuu) au +081 3340635 (ofisi ya jumuiya) e-mail: tnzncommunity@yahoo.comHABARI ZAIDI: http://www.tnzncommunity.blogspot.com


No comments:

Post a Comment