.

.

.

.

Saturday, January 10, 2009

STARS YATINGA NUSU FAINALI


Timu ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars itaivaa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars katika nusu fainali ya michuano ya soka ya Kombe la Chalenji baada kushika nafasi ya pili kwenye kundi A kutokana na kulazwa na wenyeji Uganda, The Cranes 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini hapa. Kwa matokeo hayo, Stars ilijikuta ikiambulia nafasi ya pili katika kundi hilo ikiwa na pointi sita kama Rwanda lakini iliweza kusonga mbele kutokana na kufungwa mabao machache zaidi. Stars imefungwa mabao manne wakati Rwanda itakuwa katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi sita kutokana na kupachikwa mabao sita. Inaivaa Harambee Stars kesho kutokana timu hiyo kuweza kukamata uongozi wa Kundi B kwenye Uwanja wa Nelson Mandela. Uganda iliweza kukamata usukani wa kundi kwa kuwa na pointi saba, ambapo sasa inatazamiwa kuivaa timu ya taifa ya Burundi, Indamba iliyokamata nafasi ya pili katika kundi B katika mchezo utakaofanyika pia kesho katika uwanja huo.

No comments:

Post a Comment