MASHABIKI wa Yanga wanaotaka kwenda Cairo, Misri kwa ajili ya kuishangilia timu hiyo wanatakiwa kulipa dola 800 Sh1.04 milioni.
Yanga itapambana na Al-Ahly ya Misri Ijumaa Machi 13 kwenye Uwanja wa Taifa ulioko Cairo ikiwa ni mchezo wa wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mabingwa hao wa Tanzania wamefuzu baada ya kuitoa Etoile d’Or Mirontsy ya Comoro kwa jumla ya mabao 14-0 na kuweka historia.
Mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ni nauli ya kwenda Misri na kurudi Dar es salaa pamoja na viza tu.
Madega alisema bado wanawasiliana na Misri ilikujua mambo ya hotel yatakuwaje japo kila shabiki anatakiwa kujilipia malazi na chakula.
Alisema mashabiki wote wanaotaka kwenda huko wanatakiwa kumuona Katibu Mkuu wa Yanga Lucas Kisasa kwa maelezo zaidi.
Aliongeza kuwa fomu hizo zinaanza kutolewa kuanzia leo na mwisho wa kuchukua fomu na kuthibitisha ni siku sita kabla ya safari hiyo ya Cairo.
''Bado hatujajua mechi inachezwa lini kwa kwa sababu mpaka sasa wapinzani wetu hawajatutumia barua ya kutujulisha ila tunadhani timu itaondoka hapa Machi 8 au 9 kwenda huko,'' alisema Madega.
No comments:
Post a Comment