.

.

.

.

Tuesday, February 24, 2009

JOYCE MUJURU MATATANI

Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joyce Mujuru anakabiliwa na shutuma za kufadhili biashara haramu ya kuuza dhahabu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika masoko ya Ulaya.
Bi Mujuru ambaye aliteuliwa miaka mitano iliyopita kuwa makamu wa rais, hajajibu shutuma hizo.
Yeye ni miongoni mwa vigogo wengine 200 wa Zimbabwe ambao wamewekewa vikwazo vya kimataifa kwa madai ya kukiuka haki za binadamu.
Kwa mujibu wa kampuni moja yenye ofisi zake barani Ulaya, Firstar, binti wa makamu huyo wa rais, Nyasha del Campo alinuia kuuza tani tatu unusu za dhahabu kutoka DRC.
Binti huyo, del Campo alikataa kutamka lolote huku akisema anawasiliana na mawakili wake.

No comments:

Post a Comment