.

.

.

.

Wednesday, February 18, 2009

LIYUMBA APEWA DHAMANA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa dhamana kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, anayekabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya Sh 221,197,299,200.95, baada ya kuwasilisha hati ya nyumba yenye thamani ya Sh 800,820,000. Liyumba na mwenzake, Deogratius Dawson Kweka aliyekuwa meneja wa mradi wa ujenzi wa maghorofa pacha ya BoT, wanashitakiwa kwa makosa tofauti, yakiwemo matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara. Katika masharti ya awali yaliyotolewa mahakamani hapo, yalimtaka kila mshitakiwa kutoa hati yenye thamani ya Sh. bilioni 55. Kiasi alichotoa Liyumba jana ni sawa na asilimia 1.4 ya dhamana iliyowekwa na mahakama hiyo. Kwa hali hiyo, hati iliyowasilishwa jana mahakamani hapo, ilikuwa pungufu ya zaidi ya Sh. Bilioni 54, ikilinganishwa na thamani iliyotamkwa katika masharti ya awali. Muda mfupi baada ya kuwasilisha hati hiyo, Liyumba, alikumbatiana na ndugu, jamaa na marafiki zake kwa furaha, kisha aliondoka mahakamani hapo kwa kutumia gari aina ya Toyota Land Cruiser VX.
Picha na habari kwa hisani ya IPPMEDIA

No comments:

Post a Comment