.

.

.

.

Saturday, February 07, 2009

MWANAFUNZI AUWAWA NA KUNYOFOLEWA SEHEMU ZA SIRI

MWANAFUNZI wa Darasa la Pili katika shule moja ya msingi wilayani Geita mkoani Mwanza, ameuawa kikatili kwa kunyongwa shingo yake na kisha kunyofolewa viungo mbalimbali vya mwili wake ikiwamo sehemu zake za siri. Kwa mujibu wa habari za kipolisi zilizopatikana wilayani hapa, tukio hilo lilitokea hivi karibuni na kabla ya mtoto huyo kuuawa, aliingiziwa shati lake la shule katika sehemu zake za haja kubwa, wakati kaptula yake ikiingizwa mdomoni mwake.
Katika hatua nyingine wananchi wenye hasira kali wamemkamata na kisha kumuua kwa kumpiga kwa mawe na marungu, bibi wa mwanafunzi huyo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanafunzi huyo ambaye baada ya kuhojiwa na wananchi hao, alikiri kumuua na kisha kunyofoa viungo vyake. Akithibitisha kuwapo kwa mauaji hayo ya kutisha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow, alisema mwanafunzi huyo alikuwa akisoma Shule ya Msingi Mshinde, akiwa na umri wa miaka tisa, mkazi wa Kijiji hicho cha Msinde.
Akisimulia mkasa huo, Kamanda Rwambow alisema siku ya tukio mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani asubuhi kwenda shuleni, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, hakurejea nyumbani mchana kama kawaida na hadi jioni ya siku hiyo. Alisema wazazi wake walimtafuta bila mafanikio na siku ya pili waliamua kwenda kutoa taarifa Polisi; na baada ya wananchi kupata taarifa walimwendea bibi yake aliyekuwa akiishi naye. Alisema walimweka chini ya ulinzi na kumhoji kuhusu kupotea kwa mwanafunzi huyo, na alidai aliona sehemu inayoonyesha mburuzo wa kitu wakati anamtafuta. Baada ya kufuatilia mburuzo huo waliukuta mwili huo ukiwa kichakani.
Alisema mwili huo ulikuwa umeharibiwa vibaya kutokana na kunyofolewa sehemu za siri, visigino vya miguu yote, vidole gumba vya miguu yote, macho na masikio, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida kaptula yake ya shule ikiwa imeingizwa mdomoni mwake wakati shati likiingizwa katika sehemu yake ya haja kubwa. Hali hiyo ilionekana kuwakasirisha wananchi hao na kuamua kumhoji bibi Kizee huyo, Baluli Kitando (70); na kisha alikiri kuhusika katika mauaji ya mwanafunzi huyo na kuchukua viungo vyake. Alipotakiwa kueleza alipopeleka viungo hivyo, ajuza alikataa katakata hali iliyowafanya wananchi hao kumshambulia kwa mawe hadi kumuua na kisha kukatakata viungo vyake vipande vipande na kuvitelekeza kichakani huku wakiuchukua mwili wa mwanafunzi huyo na kuupeleka nyumbani kwa maziko. Polisi walipofika katika eneo la tukio, walikuta tayari wananchi wamemaliza kumuua kikongwe huyo na kutawanyika huku mwili wa mwanafunzi ukiwa umehifadhiwa nyumbani kwao, na waliufanyia uchunguzi na kuruhusu uzikwe.

No comments:

Post a Comment