.

.

.

.

Thursday, February 12, 2009

PINDA ASEMA HOSEA NA MWANYIKA WANAWEZA KUSHITAKIWA

SERIKALI imesema kuna uwezekano wa kuwafikisha mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea ikibainika kuwa walikosea wakati wa kupitisha zabuni tata ya umeme wa dharura iliyoipa ushindi kamapuni ya Richmond.
Akitoa kauli ya serikali juu ya utekelezaji wa maazimio ya bunge kuhusiana na kashfa ya Richmond Development LLC, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kuwa uchunguzi bado unaendelea dhidi ya vigogo hao.
“Kwa sasa kazi hiyo inayoendelea ni vyombo vya dola kufanya uchunguzi zaidi, ili kuona kama kuna makosa yoyote ya jinai yaliyotendwa,” alisema Pinda.
Alisema kuwa ripoti ya uchunguzi huo ndiyo itakayoipa serikali dira ya hatua za kuchukua, kama vile kupelekwa mahakamani au hatua za kinidhamu.
Mbali na vigogo hao wawili, Pinda aliwataja wengine ambao wapo kwenye uchunguzi kuwa ni Wakili wa Serikali, Donlad Chidowu na wajumbe wa kamati za wataalamu na majadiliano, ambazo inawahusisha maofisa waandamizi wapatao 12 kutoka wizara na taasisi za umma.

No comments:

Post a Comment