VIONGOZI mashuhuri watano duniani wakiwemo Rais wa China Hu Jintao na Katibu Mkuu wa Umoja Ban Ki- Moon wanatarajiwa kufika nchini mwezi huu ili kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Wageni hao pia watakagua miradi ya maendeleo na kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na nchi zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alisema ujio wa wageni hao utakuwa wa manufaa kwa watanzania na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Akifafanu alisema pamoja na Rais wa Zambia Rupiah Banda kuwa nchini tangu jana, Rais wa China atawasili Februari 14 wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, atawasili nchini Februari 25.
Membe alisema viongozi wengine watakaotembelea nchi ni Rais wa Uturuki Abdullah Gul na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Kamalesh Shama.
Kuhusu ujio wa Rais wa China , Membe alisema kutokana na urafiki kati ya nchi hizo, Rais huyo anakuja kwa lengo la kuangalia miradi iliyofadhiliwa na nchi yake pamoja na kupanga mikakati mipya ya kuboresha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara baina ya nchi mbili
No comments:
Post a Comment