.

.

.

.

Wednesday, March 25, 2009

ALIEMPIGA KOFI RAIS MSTAAFU ALAZWA WODI YA VICHAA


IBRAHIM Said, 26, ambaye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kumpiga kibao rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa wa akili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Magereza kukanusha taarifa kuwa kijana huyo anaugua.
Awali, vyombo vya habari viliripoti kuwa afya ya kijana hiyo si nzuri gerezani. Mama wa kijana huyo alikwenda kwa Mufti Shaaban Simba kumsihi amuombe Alhaji Mwinyi pamoja na Rais Jakaya Kikwete wamnusuru mwanae na kifungo hicho, akidai kuwa alimkuta kwenye hali mbaya alipoenda kumtembelea gerezani.
Magereza ilikanusha madai hayo kwa kusema kuwa afya ya Ibrahim ni nzuri na anaendelea na kifungo chake bila ya matatizo yoyote.

No comments:

Post a Comment