Mkurugenzi wa Benchmark waandaaji wa Bongo Star Seach Ritah Paulsen akizungumza na wanahabari katika mako makuu ya Vodacom jengo la PPF Tower wakati alipoongea na wanahabari kuelezea juu ya shindano la BSS linalotarajiwa kufanyika jumamosi na jumapili mkoani Dar es alaam kulia ni Nector Foya meneja mawasiliano Vodacom
Shindano la kutafuta wawakilishi wa mkoa wa Dar es alaam katika shindano la BSS 2009 litafanyika kuanzia jumamosi mpaka jumapili wiki hii katika ukumbi wa New World Cinema ambapo zaidi ya washiriki wapatao 2000 wanatarajia kujitokeza ambapo mshindi wa mwaka huu anatarajiwa kuondoka na zaidi ya milioni 15 ambazo mshindi wa mwaka jana alijishindia.Kampuni ya simu za mkononi Vodacom ni wadhamini wa shindano hilo linaloratibiwa na kampuni ya Benchmark Production ambapo zaidi ya vijana 8000 wameshiriki katika mchujo huo mikoani kote ambako shindano hilo limefanyika na vijana 35 wameingia raundi ya pili .
No comments:
Post a Comment