Baada ya hadithi za miaka teleee...hatimaye serikali la Mh. Raisi JK.....liko kwenye mchakato wa ukweli kwa ajili ya ujenzi wa wanja kubwa kabisa la kisasa la midege (EYAPOTI) kitakachokidhi mahitaji ya usafiri wa anga katika miaka 50 ijayo. Taarifa iliyotufikia imedai kuwa mpaka sasa serikali imebaini sehemu 2...maeneo ya Mkoa wa Pwani ambayo yanaweza kujengwa kiwanja hicho kitakachokidhi mahitaji . Kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya Miundombinu,maeneo hayo yako Bagamoyo na Mkuranga ambapo taratibu za kuyapima na kupata hati zinafanywa na wizara hiyo, kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege. Sambamba na hatua hiyo serikali inao mpango wa muda mrefu wa kuendeleza Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ambapo hivi sasa inakamilisha mazungumzo na Kampuni ya kimataifa kutoka China ya China Sonangol kwa ajili ya kupanua na kuendeleza kiwanja hicho.
Kazi ya usanifu na upanuzi wa kumbi za kuondokea na kufikia wageni katika uwanja huo ilikuwa imeshaanza na inafanywa na Mhandisi kutoka Kampuni ya Aeroproject hapa Town na inatarajiwa kukamilika mwezi huu.
Si wanunue midege kwanza kodi za uwanja tu hazitoshi!
ReplyDelete