.

.

.

.

Monday, April 20, 2009

DECI MAHUTUTI !!!

SIKU chache baada ya kusimamishwa shughuli za Taasisi ya Development Enterpreneurship Community Initiative (Deci), serikali imetangaza kufunga akaunti zote za wamiliki wake na kudhibiti maeneo yote ya shughuli za taasisi hiyo kwa lengo la kuwezesha kurudisha fedha kwa wananchi.
Tamko hilo la Serikali limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo katika mkutano na waaandishi wa habari makao makuu ya wizara hiyo huku waziri huyo akiwaweka waandishi ukumbi wa mikutano kwa zaidi ya saa moja na nusu kumsubiri.
Kauli hiyo ya Serikali imekuja wakati wanachama wa taasisi hiyo wakiwa katika hali tata kutojua hatima ya mbegu zao walizopanda wakati wakisubiri hatima ya uchunguzi wa serikali.
Waziri Mkulo aliyeelezwa kuanza mkutano saa sita na robo, mchana aliingia ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo saa 7. 48 na kueleza kuwa " Tamko nitakalolitoa ni zito na muhimu, limepitiwa na kukubaliwa na Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais. Mimi natoa tamko la serikali kama waziri kwa ababu shughuli za taasisi hiyo zinaihusu wizara yangu ya Fedha na uchumi:
"Ilibidi wakubwa walipitie na kuidhinisha, ni tamko linalojitosheleza kwa kila hali, lina kurasa 21, lakini hapa nimefupisha hadi kufikia kurasa tatu,"alisema Mkulo.

Alisema Deci imeamua kusitisha shughuli zake hatua ambayo imesababisha wasiwasi mwingi miongoni mwa wanachama wake na kwamba serikali imeamua "Kuhakikisha maeneo yote ya shughuli za Deci yanadhibitiwa, kukinga pesa zote zilizopo katika akaunti za waendeshaji wa Deci na Deci yenyewe hadi hatma ya shughuli za Deci itakapojulikana."
Waziri Mkulo alibainisha kuwa "Serikali inaendelea na hatua za kuhakikisha waendeshaji na wamiliki wote wa Deci hawatoroki."

No comments:

Post a Comment