.

.

.

.

Wednesday, April 29, 2009

KAMA ILIYOANDIKWA NA www.lukwangule.blogspot.com

HALI katika hospitali ya wilaya ya temeke ni ya kutisha, kutia huzuni na pia kusikitisha.Madaktari na wauguzi wamekuwa wakichemka vikali kusaidia wagonjwa mbalimbali waliotokana na milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi Mbagala.Dk Mahita alimwambia mwandishi wa habari hizi ambaye naye alifika hospitalini hapo pamoja na kuandika habari kuangalia watoto wake ambao mpaka jioni walikuwa hawajulikani walipoalisema kwamba mpaka saa kumi na nusu kulikuwa na majeruhi zaidi ya 155 waliofikishwa katika hospitali hiyo wengi wao wakiwa na hofu na kuzimia.Aidha Dk Mahita alisema mpaka muda huo alikuwa na maiti watatu mmoja akiwa mtoto.Ingawa alisema kwamba kila kitu kinaendelea vyema lakini ni wazi idadi ya wauguzi na kasi yakuingia kwa wagonjwa ilionyesha kuwaelemea wauguzi wa hospitali hiyo kiasi cha mkuu wa mkoa William Lukuvi aliyefika hapo kuamua kupiga simu kuomba msaada.Huku maelfu ya wananchi wakiwa wanaendelea kumiminika katika hospitali hiyo na kuzuiwa navikosi vya askari wa kutuliza ghasia wakisaidiwa na mbwa,magari ya kubeba wagonjwa na ya watu binafsi yalikuwa yakiingia na kutoka.Wengi walikuwa wameletwa wakiwa na hali mbaya ya mfadhaiko wengine wakiwa kama wamepigwana shoti.Mmoja wa maiti inadaiwa kwamba alikatwa vipande viwili na mabomu.Kitu ambacho kilionekana dhahiri katika mapokezi ni udogo wa sehemu hiyo ambapo ilikuwa nuikupokea wagonjwa kuangalia wana nini kuwapiga dripu na kisha kuwakimbiza.Dk mahita alisema kwamba walikuwa wanafanya mipango ya kupata eneo jingine la kutunza wagonjwa kwani hospitalini hapo palikuwa pamejaa.Watu waliokuwa wanataka kuwaona wagonjwa wao wa kawaida hospitalini hapo walishindwa kuingia katika hospitali kutokana pilikapilika za majeruhi na hofu ya usalama kwamba wakiruhusu maelfu ya wtau waliopo nje wanaotafuta ndugu na watoto watavamia hospitali na itakuwa taabu kubwa kuwaondoa.Mkuu wa mkoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi amesema kwamba moto umedhibitiwa katika hanga ambako mambomu yamelipuka ingawa anasema kwamba hawawezi kuwa na uhakika wa fukuto lililopo.Hata hivyo amesema hanga jingine ambako kuna makombora lipo salama.Serikali ilikuwa inatarajia kutoa taarifa yake jana jioni.Zifuatazo ni picha mbalimbali nilizopiga hospitali ya Temeke.

No comments:

Post a Comment