Hakuna shabiki wa muziki asiyefahamu kwamba msanii Lucas Mkenda a.k.a Mr. Nice kuwa aliwahi kuitikisa Afrika Mashariki kwa ngoma zilizowapagawisha wengi, hata mitaani kwetu na sehemu nyingine tulipokuwa tukikatiza tulikutana na baadhi ya watoto wakiimba nyimbo hizo kama Kikulacho, Kidali po na Baba lao FAGILIA.Tunachotaka kusema ni kwamba, baada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye game huku akiwaacha mashabiki wake njia panda, mchizi amerudi tena, mkononi akiwa na albamu yenye jina la ‘Wakinuna’ ambayo ina jumla ya nyimbo saba itakayozinduliwa Aprili 12, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Maisha Club uliopo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment