MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea jana alikuwa kwenye wakati mgumu baada ya wabunge kumhoji uhalali wake wa kuiongoza taasisi hiyo wakati akikabiliwa na tuhuma za kusafisha kashfa ya zabuni ya mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura.
Mkurugenzi huyo, ambaye alitajwa kwenye taarifa ya tume teule ya bunge iliyochunguza kashfa hiyo na serikali kutakiwa kumchukulia hatua, alikumbwa na mtafaruku huo katika semina ya Miundombinu ya Uadilifu iliyoandaliwa na Takukuru na Chama cha Wabunge wa Afrika (APNAC) na kufanyika kwenye hoteli ya Whitesands jijini Dar es salaam.
Ilifikia wakati Dk Hosea alionekana kukerwa sana na maswali kiasi cha kulazimika kuwaonya kuwa anao uwezo wa kuwachafua kama wakiendelea kufanya mambo yanayoonekana kumvua nguo.
Ilifikia wakati Dk Hosea alionekana kukerwa sana na maswali kiasi cha kulazimika kuwaonya kuwa anao uwezo wa kuwachafua kama wakiendelea kufanya mambo yanayoonekana kumvua nguo.
Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni ndiye aliyeanzisha kizaazaa hicho baada ya kumhoji Dk Hosea akisema ilikuwaje taasisi yake iliisafisha kampuni tata ya kuzalisha umeme wa dharura Richmond Development (LLC) iliyokuwa inakabiliwa na kashfa ya kushinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura wakati kamati teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza mkataba wake, iligundua kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
“Inakuwaje wakati wa mjadala wa Richmond, wewe mkururugenzi wa Takukuru ulikanusha kuwapo rushwa na uchunguzi wa kamati ya bunge ulibaini kuwepo rushwa ndani ya kampuni hiyo? Je ni nani mwenye dhamana ya kukuadhibu wewe na taasisi yako kuhusu rushwa’’ aliuliza Chageni.

Swali hilo halikutegemewa na Dk Hosea na lilionekana kumuudhi na kulazimika kuchukua kipaza sauti na kusitisha maswali na kuanza kujibu kwa ghadhabu.
“Hapa siyo jukwaani hivyo tusilete siasa. Nipo hapa kwa ajili ya kufundisha na kama ni suala la Richmond waziri mkuu alishaliongelea na ndiyo mwenye dhamana ya kujibu hilo. Mimi sina jibu kwa hilo na kama mtu hapendi kuvuliwa nguo kwanini umvue mwenzako,” alisema Dk Hosea.

"Mjadala huu aachiwe Waziri Mkuu Mizengo Pinda na aliyeuliza swali hilo hanitendei haki kwani hakuna hoja nyingine ya maendeleo kwa jamii ambalo inaweza kujadiliwa... mbona mnang’ang’ania kujibu hilo pekee.
“Najua kuna watu wanatumiwa ili niongee halafu nibabaike katika kujibu na nishindwe kufanya kazi yangu. Mbona mnang’ang’ania jambo hilo tu wakati kuna hoja nyingine za maendeleo kwa jamii. Kuhusu suala la Richmond sijibu ng’o.”.

Yeye ndio anayengángánia hapo! manake angekuwa na busara angekuwa alishajiuzuru siku nyingi!! Hakuna hakuna fedheha kubwa kama iliyofanywa na TAKUKURU chombo ambacho kimepewa dhamana ya kupambana na kuzuia ndio kinakuwa mtetezi wa mafisadi yasiyo na huruma hatakidogo kwa wananchi wake! Eti hakuna mazingira ya rushwa yaliyotumika kumpata mzabuni Mlitumia nyaraka gani! That is selfish ya hali ya juu!!!!!
ReplyDelete