.

.

.

.

Friday, May 01, 2009

MH.CHENGE AONGEZEWA SHITAKA LA NNE





MBUNGE wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), ameongezewa shitaka la nne badala ya matatu yanayomkabili katika kesi ya kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili.
Katika shitaka hilo la nne, alilosomewa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Chenge anadaiwa kuendesha gari bila kuwa na hati ya bima.
Kutokana na kuongezwa shitaka hilo, alisomewa upya mashitaka yanayomkabili.
Mwendesha Mashitaka Mkuu, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), David Mafwimbo wa mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi, Emiliusi Mchaulo alisema kuwa katika shitaka la kwanza, Chenge anadaiwa kusababisha kifo cha Victoria George kwa uendeshaji wa gari kizembe.
ASP Mafwimbo alidai kuwa Machi 27, mwaka huu, majira ya saa 10:30 alfajiri, katika barabara ya Haile Selassie, Wilaya ya Kinondoni mshitakiwa huyo, akiwa anaendesha gari yenye namba za usajili T 13 ACE, aina Toyota Hilux Double Cabin, kwa uzembe na kushindwa kuchukua tahadhari kama inavyotakiwa kwa watumiaji wa barabara, aligonga bajaj yenye namba za usajili T 739 AXC na kusababisha kifo cha Victoria ambaye alikuwa abiria katika bajaj hiyo.
Katika shitaka la pili, Mafwimbo alidai, Chenge anadaiwa siku na muda huo huo, alisababisha kifo cha Beatrice Constantine kwa kuendesha gari kizembe na la tatu ni kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa bajaj ambayo ilikuwa imebeba wanawake hao.
Na shitaka la nne ambalo ndilo ameongezewa jana, ASP Mafwimbo aliiambia mahakama kuwa ni kuendesha gari bila kuwa na hati ya bima. Chenge alikana mashitaka hayo.
Kabla ya kupanda kizimbani na kusomewa mashitaka hayo, Chenge aliyeongozana na wakili wake, aliingia katika chumba cha mahakama mapema, huku akisubiri kupanda kizimbani kusomewa mashitaka yake

No comments:

Post a Comment