.

.

.

.

Friday, May 08, 2009

WANASWA NA MADAWA YA KULEVYA

JESHI la Polisi kupitia kitengo cha dawa za kulevya linawashikilia wanawake wawili kwa tuhuma za kupatikana na mihadarati. Shirima Ally (58), mkazi wa Forodhani na Jang’ombe, Zanzibar, alikamatwa juzi saa nne asubuhi katika eneo la bandari ya Dar es Salaam, akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilo moja, akiwa katika harakati za kuzisafirishwa kwenda Zanzibar. Kamanda wa Polisi wa Kitengo hicho, Kamishna Msaidizi wa Polisi Godfrey Nzowa, alithibitisha kukamatwa kwa mwanamke huyo, ambaye alikuwa ameficha dawa hizo kwenye mfuko wa nailoni na kuziweka ndani ya mkoba uliofunikwa na nguo. Nzowa alisema walipomhoji Shirima alidai dawa hizo si zake, bali alipewa na rafiki yake waliyekutana mjini Dar es Salaam, ili ampelekee nyumbani kwake Zanzibar, kwa madai kwamba yeye angekwenda siku nyingine. Alisema Shirima alidai hakujua kama kilichokuwa ndani ya mfuko huo ni dawa za kulevya, bali alidhani ni bidhaa za kawaida ambazo ni kwa matumizi ya nyumbani. Kamanda Nzowa alimtaja rafiki huyo kuwa Anna Zanganya (36), mkazi wa Mabibo, Dar es Salaam aliyekamatwa juzi saa 12:30 asubuhi akiwa na mabunda 47 ya mirungi, katika eneo la bandari ya Dar es Salaam. Alisema sawa na Shirima, mwanamke huyo alikuwa akisafirisha mirungi hiyo kwenda Zanzibar. Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na ushirikiano kati ya polisi na raia wema waliotoa taarifa. Alisema jeshi limejipanga vyema katika kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya. Kamanda Nzowa ametoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa za wauzaji, wasambazaji, watumiaji na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ili watiwe nguvuni.

No comments:

Post a Comment