.

.

.

.

Friday, May 01, 2009

WAZEE YANGA WAMKOMALIA MENGI

WAZEE wa Yanga, wamechukizwa na kauli za Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi za kumtuhumu mfadhili wa klabu hiyo, Yusuf Manji kuwa ni mmoja wa 'mafisadi papa' wanaoitafuna nchi.Kutokana na matamshi hayo, wazee hao walisema wanamtaka, Mengi kumwomba radhi Manji pamoja na wanachama wote wa Yanga ambao wamefedheheshwa na kauli hiyo.Pia walitaka Serikali kumchukulia hatu za kisheria Mwenyekiti huyo kutokana na kauli zake hizo.Wakizungumza Dar es Salaam jana na waandishi wa habari, Wazee hao walisema baada ya kuzitathimini kwa kina tuhuma hizo, wamegundua ni za kupika zenye dhamira ya kumchafua Manji.Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Yahya Akilimali alisema watu wengi wanafahamu, Mengi hakuondoka Yanga vizuri, kwani aliondoka kutokana na wanachama kumkataa kuwa pamoja naye katika usuluhishi wa mgogoro uliokuwa umejitokeza wakati huo."Manji alikuja Yanga akiwa na busara za hali ya juu na hekima za kutosha, aliwakutanisha na kuwapatanisha, kitu ambacho alifanikiwa na sasa Yanga, ipo shwari na kaifanyia mambo makubwa klabu yetu," alisema Akilimali.Akilimali alisema wana-Yanga, wana amini chimbuko la wivu na chuki za Mengi ni pamoja na kuona, Manji ameweza kufanikiwa pale aliposhindwa yeye, kwani kuanzia wakati huo amekuwa akimfuatilia mfadhili huyo.Alisema tuhuma hizo zinalenga ubaguzi wa rangi, kitu ambacho duniani kote kinapigwa vita na hata hayati, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akilaani vitendo vya ubaguzi wa rangi na pia aliwahi kuonya kwa kusema, "dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu," alikariri baadhi ya maneno ya Nyerere.Naye Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuph Mzimba alisema, Mengi alitakiwa kufuata taratibu za kisheria kama kweli ana ushahidi na anachokiongea na si kuwakashifu watu wengine.

No comments:

Post a Comment