.

.

.

.

Monday, June 01, 2009

MRADI MKUBWA WA MAJI MKOANI SHINYANGA


RAIS Jakaya Kikwete amezindua mradi mkubwa wa maji kuliko yote Kusini mwa Jangwa la Sahara wa Ziwa Victoria ambao umegharimiwa na Serikali ya Tanzania bila ya msaada wa wahisani kwa zaidi ya Sh bilioni 200.Uzinduzi huo ulionyeshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa,TBC1.Katika hotuba yake ya uzinduzi uliofanyika wilayani Misungwi mkoani Mwanza jana, Rais Kikwete alisema uzinduzi huo ni sehemu tu ya utekelezaji wa ahadi za serikali yake kwa wananchi .Alisema mradi huo ni kielelezo cha dhamira ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza ahadi zake za kuwapatia wananchi maji safi na salama.Aidha alimsifu Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliyekuwapo katika uzinduzi huo kwa uthubutu wa kuamua kuanzishwa kwa mradi huo.“Ndani ya Ilani ya CCM, mradi huu ulipaswa kukamilika mwaka 2010, Rais Mkapa alituachia na akaamini tutaweza na kweli Serikali ya Awamu ya Nne imekamilisha mradi huo kabla ya wakati uliokuwa umepangwa.“Hii inadhihirisha CCM inaweza. Tumewaweza Busanda na bado tutaendelea kushinda, na mradi huu ni ushahidi,” alisema Rais Kikwete.Pichani:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza msichana Martha Philipo kutoka katika kijiji cha Iselamagazi,Shinyanga, mara baada ya kuteka maji na kumtwisha ndoo wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha kuchotea maji iliyofanyika kijijini hapo jana jioni.Kituo hicho cha kuchotea maji ni moja kati ya vituo vingi vya kuchotea maji vilivyo katika mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga.Pembeni ya Rais ni Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya.Picha nyingine Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua bomba la maji katika kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Iselamagazi wakati wa hafla ya kufungua kituo hicho iliyofanyika katika kijiji hicho jana mchana.Pia Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa na Waziri wa Majui Profesa Mark Mwandosya wakizungumza wakati wakikagua mitambo mikubwa ya kusafisha maji iliyopo katika kijiji cha Ihelele Wilaya ya Misungwi jana mchana.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa nmdiye aliyeasisi mradi huo mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga

No comments:

Post a Comment