Filamu ya Hostel iliyochezwa na mastaa mbalimbali wanaofanya vyema katika game hiyo tayari imedondoka kitaani kupitia Kampuni ya Tuesday Entertainment.Ndani ya safu hii, mwandaaji wa muvi hiyo, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuzi’ alisema kwamba, filamu hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa fani hiyo nchini imeingia kitaani ikiwa katika DVD, VCD na VHS.“Baadhi ya wasanii walioshiriki kwenye filamu hiyo ni pamoja na Mohamed Mwikongi ‘Frank’, Aunt Ezekiel, Ahmed Olutu ‘Mzee Chilo’, Mariam Jolwa ‘Jini Kabula na wengine wengi,” alisema Chuzi.
No comments:
Post a Comment