.

.

.

.

Friday, July 10, 2009

WAKUTWA NA MANOTI FEKI

Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kupatikana na dola bandia za Kimarekani 340,000 ambazo kwa mahesabu ya haraka haraka ni sawa na billioni nne na ushee za Kitanzania.Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kikondoni, Mark Kalunguyeye amesema watu hao walikamatwa jana katika chumba namba 116 kwenye hoteli ya Pipolo Mbezi Jijini.Amewataja waliokamatwa kuwa William Kinde , 36, Luhinda, 43 na Emmanuel Petro, 40. Kamanda amesema Luhinda alikuwa akidanganya kuwa yeye ni rubani wa ndege za kimataifa.Akasema watu hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
CHANZO: ALASIRI

No comments:

Post a Comment