Wanasayansi kutoka Marekani wamegundua kuwa theluji na barafu katika mlima mrefu barani Afrika, Kilimanjaro uliopo nchini Tanzania inayeyuka kwa kasi na huenda ikatoweka ndani ya miaka 20.Utafiti huo ambao umechapishwa katika jarida la Proceedings of the National Academy of Sciences, ulikuwa wa kwanza kujua kiwango cha barafu kilichopotea katika mlima huo. Umegundua kuwa tandiko kuu la barafu hiyo lilisinyaa kwa asilimia themanini na tano tangu mwaka 1912.Barafu nyingine ilisinyaa kwa zaidi ya asilimia hamsini katika kipindi cha miaka tisa iliyopita.
Utafiti huo umebaini kuongezeka kwa joto la dunia huenda ikawa ndio sababu ya kuyeyuka kwa theluji hiyo.
No comments:
Post a Comment