Kiota cha kujiachia cha Maisha Club kilichopo Oysterbay jijini Dsm leo mchana kimeteketea kwa moto, taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wamesema kuwa kulikuwapo na ukarabati uliokuwa unaendelea wa vipupwe (AC),kwa bahati mbaya wakati wa ukarabati huo mojawapo ikalipuka kutokana na nyaya zake kugusana,na baadaye moto mkubwa ukazuka katika jengo hilo,imeelezwa kuwa taarifa zilifika kwa watu wa zima moto lakini hawakuwahi kuuzima moto huo kwa haraka kwani kwa asilimia kubwa vitu vilivyokuwemo vilikuwa vimekwishateketea.
No comments:
Post a Comment