.

.

.

.

Wednesday, February 24, 2010

JOTI WA ZE KOMEDI ALAZWA MOI BAADA YA .....


Msanii maarufu wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi,Lukac Mhavile a.k.a Joti (pichani) anahofiwa kuvunjika shingo,baada ya kupata ajali alipokuwa akirekodi kipindi pamoja na wenzake eneo la daraja la Salender,jijini Dar.Joti aligongwa na lori aina ya Scania malai ya Ubalaozi wa Ubelgiji nchini,saa 5:30 jana asubuhi.Amelazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa matibabu,akiwa amefungwa kifaa maalum cha kuzuia shingo kukunja na kugeuka.Akizungumzia tukio hilo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni,Sebastian Masinde,alisema ajali hiyo ilitokea wakati msanii huyo akiwa na wenzake wakiigiza tukio lililodaiwa kutokea eneo hilo la Mwanamke kuoata Manyoya baada ya kumpa ombaomba pesa.Alisema walipokuwa wakiigiza wakiwemo pia wasanii wenzake Masanja na Mpoki,ombaomba waliokuwa karibu walichachamaa na kuwazuia wasiigize ambapo katika kufanya hivyo waliwavamia na Joti na wenzake wakalazimika kukimbia."walipokuwa wakikimbia ndipo alipogongwa na gari,wamekasirika kwa sababu sasa mwenye kila gari lake anayepita pale anafunga vioo,hivyo hawakupenda Komedi waigize tukio hilo na kuanza kuwafukuza.kamanada Masinde alisema kuwa baada ya tukio hilo, Majeruhi walipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amelazwa MOI,na dereva wa Lori hilo anashikiliwa na polisi pamoja na gari lililosababisha ajali hiyo.

1 comment:

  1. pole joti,but those beggars had no raeson to do dat to joti,but it happened,may god bless you.

    ReplyDelete