.

.

.

.

Tuesday, March 23, 2010

WAFUNGWA MAISHA KWA KUBAKA

WAKAZI wawili wa jijini Dar es Salaam, Januari Protus maarufu kama Soko (28) na Said Mohamed (22), wamehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 20.

Akituo hukumu hiyo jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Hakimu Pamela Kalala alisema baada ya kusoma ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi uliotolewa na washtakiwa wenyewe, watatumikia kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, wakili wa Serikali, Credo Lugaju aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa vijana wenye tabia kama hiyo.

Washtakiwa walipotakiwa kujieleza kwanini wasipewe adhabu kali na Hakimu Kalala, waliiomba mahakama iwapunguzie adhabu kwa madai hilo ni kosa lao la kwanza na kwamba wanategemewa na familia zao.

Hakimu Kalala alitoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka ukiwepo wa msichana huyo aliyebakwa.

Msichana huyo, alidai siku ya tukio alikuwa akitoka nyumbani kwao mkoani Kirimanjaro na kushuka katika stendi ya mkoa ya Ubungo.

Alisema baada kuchukua teksi kuelekea Kariakoo na kuteremka aliktana na Januari ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake na pia mzazi mwenzie na kumuuliza kwanini alimchoma nyumba yake moto iliyopo katika mtaa wa Mchikichini wilayani Ilala.

Alidai baada ya Januari kumweleza hivyo alikana kuhusika na tukio hilo, hivyo mshtakiwa alimueleza achague adhabu moja kati ya tatu alizompa kuwa ni Kumwingiza chupa sehemu za siri au kumlawiti au afanyiwe kitendo cha ngono na kundi la wanaume zaidi ya watano.

Januari alivyonipa adhabu hizo tatu nichague, nilikataa zote hivyo alinikamata kwa nguvu na kunivutia chumbani kwake na kulikuwa na kundi la vijana zaidi ya watano ambao walinibaka kwa zamu alidai muathirika huyo.

Alidai baada ya kufanyiwa tendo hilo baya alifanikiwa kuwafahamu vijana wawili kati ya watano ambao aliwataja kuwa ni mshtakiwa Januari na Said kuwa ni miongoni mwa waliohusika.

Washtakiwa hao wanadaiwa kumbaka msichana huyo Desemba 12, mwaka 2008, saa 2:00 usiku huko katika eneo la mtaa wa Mission Kota wilaya ya Ilala.

No comments:

Post a Comment