.

.

.

.

Wednesday, August 01, 2012

AUNTY EZEKIEL KUFUNGA NDOA HIVI KARIBUNI

Msanii Aunty Ezekiel, ambaye anatarajia kufunga ndoa mwezi October mwaka huu, na mpenzi wake anayeishi Dubai .

Mtandao wa DarTalk, ulifanya mazungumzo mafupi na msanii huyo juu ya maisha yake na filamu kwa ujumla ambapo, alisema kuwa ameamua kuchukua maamuzi hayo ya kutaka kufunga ndoa kwani anahitaji kuishi na mtu ambaye wataweza kupanga naye maisha.

Alidai kuwa mpenzi wake huyo ni Mtanzania ingawa anaishi nje, ambapo anaamini baada ya kufunga ndoa na yeye anataweza kwenda kufanya kazi huko.

“Nilikuwa kimya juu ishu hii lakini nachotaka kusema ni kwamba mambo yangu sasa yameanza na nimeamua kufunga ndoa, hivyo mashabiki wangu nahitaji nao waweze kujua kuwa sasa nimeamua kuchukua maamuzi hayo,” alisema.

Ezekiel alisema kuwa vikao vya harusi na kupanga itakavyokuwa wameshaaza kukaa, kwani wameanza Jumapili.

Aliongeza kuwa mbali na mchakato huo mkubwa pia mwaka huu wa 2012 kampuni yake inatarajia kufunga mwaka kwa kutoa filamu mbili ambazo anaamini zitakuwa moto wa kuotea mbali.

No comments:

Post a Comment