kutoka kushoto ni Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA), Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006)
Kikundi cha wasichana maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504.
Kikundi hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii.
Lengo la Mabalozi hawa ni kuhamasisha uchangiaji na kuwezesha kujenga zaidi ya hosteli 5 kati ya 30 ambazo TEA imepanga kujenga.
Katika Uzinduzi huo uliofanyika Tarehe 31/07/2012 katika hoteli ya Serena Jijini DSM kati ya mabalozi hao na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambapo ni Faraja Nyarandu pekee ndie alikosekana kutokana na kubanwa na majukumu mengine lakini alithibitisha uwepo wake katika kampeni zinazoendelea
No comments:
Post a Comment