.

.

.

.

Wednesday, February 06, 2013

TAIFA STARS NA INDOMITABLE LIONS UWANJANI LEO




WAKATI timu za soka za Tanzania ‘Taifa Stars’ na ile ya Cameroon ‘Indomitable Lions’ zinashuka leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, makocha wa timu hizo Mdenmark Kim poulsen wa Stars na Mfaransa Jean Paul Akono wametamba vikosi vyao kuibuka na ushindi.

Timu hizo zitakutana katika mchezo wa kimataifa uliopo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Kimatifa (FIFA), utatumika kama maandalizxi kwa timu hizo kwa ajili ya kujiandaa  na mechi zake za kuwania tiketi ya kucheza fainali ya kombe la Dunia zitakazopigwa mwakani nchini Brazil.

Wakati Stars itasaka tiketi ya kombe la Dunia kwa kucheza na  Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Cameroon inatarajiwa kukwaana na Togo. 
Akizungumza na waandishi wa habari jana,  Poulsen pamoja na kufurahi kupata nafasi ya kucheza na Cameroon kutokana, alisema kwamba kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo ambao ni muhimu kwao kwani utawasaidia sana katika maandalizi yao ya kuivaa Morocco. 
 Alisema amekuwa akihitaji mechi ngumu kama hiyo ili kujenga timu imara na kwamba amekiandaa vema kikosi chake kupitia mazoezi ya siku chache walizokaa kambini na kwa ari pamoja na utayari walionao vijana wake anaimani watafanya vema katika mchezo huo. 
 “Napenda sana kaulimbiu ya Umoja ni nguvu, wachezaji ni wamoja, sisi wote ni wamoja na hivyo wachezaji wangu wanatakiwa kucheza vizuri mchezo huu ili kuwapa changamoto Cameroon na hasa ikizingatiwa kuwa watanzania wanasubiri mambo mazuri kutoka kwao,”alisema 
Kocha huyo aliongeza kuwa anaiheshjimu Cameroon kwani ni timu nzuri na yenye wachezaji wazuri lakini hilo haliwazuiii kushinda mchezo wa leo huku wakiamini mtindo wao wa uchezaji ni kupiga pasi kwa wingi na kutengeneza nafasi na kufunga, huku wakicheza  kwa haraka na hata wakipoteza mpir wanajituma wote kuutafuta.

Naye nahodha wa Stars, Kaseja alisema kwamba wako tayari kwa mchezo huo, kinachohitajika zaidi ni umoja baiina yao ili kuweza kushinda, hivyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwaunga mkono. 
Kwa upande wa kocha wa Cameroon, Akono pamoja na kufurahi kupata nafasi ya kucheza na Stars alisema kikosi chake kiopo tayari kwa mchezo huo ambao anaamini utakuwa na ushindani mkubwa kwani Stars pia ni timu nzuri. 
Alisema mchezo wa leo si muhimu kwa Stars tu bali hata kwa timu yake ambayo pia itakuwa na kibarua cha jkucheza mechi ya kusaka kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani hivyo anaamini kila timu itacheza kwa nafasi na uwezo ilionao ili mwisho wasiku itoke na matokeo mazuri. 
Naye nahodha wa Cameroon, Pierre Wome alisema wamefurahi kuja kucheza na Stars na kwamba wachezaji wenzake wapo tayari kwa mchezo wa leo ambao utakuwa wa mwisho kwao katika maandalizi yao dhidi ya Togo mwezi Machi. 
Kikosi cha Stars kilichopo kwenye hoteli ya Tansoma kinaundwa ,makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba) ambaye ni majeruhi , Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar). 
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). 
Aidha kikosi cha Cameron kitawakosa nahodha wake Samuel Eto'oo Fills na Alexndre Song walio majeruhi hivyo kitawakilishwa na Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki Nicolas Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha wa SC Olhanense ya Ureno, beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji Fabrice Olinga wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa Udinese ya Italia ambaye yuko kwa mkopo Granada ya Hispania na beki wa kushoto Henri Bedimo wa Montpellier ya Ufaransa. 
Wengine ni Charles Itandje, Benoit Assou Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice Olinga Essono, Allam Nyam, Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Makoun, Jean Kana Biyick, Joel Matip, Vincent Aboubakar, Alexandre Song, landre Nguemo, Pierre Wome, Jean Nyontcha, Achille Emana na Charles Eloundou..
Viingilio katika mchezo huo utakaoanza saa 11 jioni sh 5,000 kwa viti vya kijani, sh 7,000 kwa viti vya bluu sh 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh 15,000 kwa VIP C, sh 20,000 kwa VIP B n ash 30,000 kwa VIP A.

No comments:

Post a Comment