Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao la Daniel Sturridge lililoipa ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United kwenye Uwanja wa Anfield. Huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Liverpool tangu kuanza kwa msimu, matokeo iliyowahi kupata miaka 19 iliyopita. (Picha kwa Hisani ya Gazeti la Daily Mail la Uingereza)
Sturridge akishangilia bao pekee la Liverpool, alilofunga leo. Ushindi huo umekuja wakati ambao mshambuliaji huyu anaadhimisha miaka 24 ya kuzaliwa kwake leo Septemba 1.
Sturridge akidondoka baada ya kupiga kichwa kufunga bao hilo akiunganisha pasi ya kichwa ya Daniel Agger aliyeunganisha kona ya Steven Gerrard.
Sturridge akikumbatiana na kocha wa Liverpool Brendan Rodgers baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi.
Mashabiki wa Liverpool wakiwa wamekaa jukwaani kuunda picha na kuandika namba 100 ambayo ini idadi ya miaka ambayo nguli wa zamani aliyezaliwa Septemba 2, Bill Shankly ilikuwa aitimize, ingawa alifariki kabla.
Steven Gerrard wa Liverpool, akitunishiana msuli na Robin van Persie wa Man United wakati wa mechi hiyo.
Martin Skrtel (37), ambaye aliingia kujaza pengo la majeryhi Kolo Toure, akiruka juu kuwania kupiga mpira wa kichwa kuondoa hatari langoni mwa Liverpool.
Steven Gerrard akipiga adhabu ndogo.
Kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson (wa pili kulia) akifuatilia mtanange huo wa kukata na shoka kwenye dimba la Anfield.
Mshambuliaji Luis Suarez wa Liverpool, akiangalia mechi hiyo akiwa jukwaani.
Kocha wa Liverpool, Rodgers (kulia) na wa Manchester United David Moyes wakitoa maelekeo kwa wachezaji wa vikosi vyao.
No comments:
Post a Comment