.

.

.

.

Wednesday, April 23, 2014

MHARIRI WA MOBLOG ALONGA

Jakaya-Kikwete1
Kutoka kwa Mhariri Mkuu wa MOblog Tanzania
Tumepokea kwa furaha kama waandishi wa habari za mtandaoni (Social Media) kwamba Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) wilayani Karatu kimefurahishwa na mchango unaotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika kuchochea maendeleo bila upendeleo.
Tunasema hivyo kwa sababu huko nyuma kulikuwa na dhana ya kwamba sehemu ambazo (Majimbo) upinzani umechukua basi serikali huwa inachelewesha maendeleo kwa makusudi kwenye jimbo husika kwa kuwa ni la wapinzani.
Sasa chama kikuu cha upinzani kimekubali kwamba dhana hiyo haipo kwani wameona wenyewe mkuu wa nchi yaani Rais Kikwete yupo kuwatumikia watanzania wote bila kujali ni dini, au rangi au chama ngani? tunachukua nafasi hii adimu kumpongeza Rais wetu kwa ukomavu anaoonyesha kwa wananchi wake.
Ndiyo bravo JK kwa kuangalia maslahi mapana ya nchi na watu wake na ndiyo maana siku zote umekuwa mstari wa mbele katika kushughulikia kero za wananchi kama vile maji, umeme, barabara, zahanati na upatikanaji wa madawa katika hospitali za rufaa nchini nzima.
Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imesema kuwa pongezi hizo zilitolewa jana mchana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Lazaro Titus Massey wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la Halmashauri hiyo mjini Karatu na Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na Chadema.
Kwa misingi hiyo basi, Rais Kikwete anahitaji pongezi za dhati kabisa kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwaletea watu wa taifa hili maendeleo na hatimaye kutoka katika dimbwi la umasikini.
Wakazi wa Wilaya ya karatu kwa maneno yao wenyewe wamesema bila ya Rais Kikwete wasingepata jengo hilo pamoja ya kwamba Halmashauri hiyo ni Chadema lakini JK akaamua kuchangia maendeleo ya Wilaya hiyo.
Taarifa zinasema kwamba jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo limegharimu Tsh 1.412 bilioni na kati ya hizo Serikali ilitoa Tsh 1.394 bilioni na Halmashauri kuchangia Tsh 18 milioni.
Akinukuliwa na vyombo vya habari Rais Kikwete amesema sera ya Serikali yake ni kusambaza maendeleo kwa watanzania wote bila kujali misimamo yao ya kisiasa wala kuongozwa na hisia nyingine mbali na ukweli kuwa kila mtu anataka maendeleo.
Damas Makangale
Mhariri Mkuu MOblog Tanzania

No comments:

Post a Comment