.

.

.

.

Friday, July 25, 2014

MASHAUZI CLASSIC KUZINDUA ALBAM MPYA IDD MOSI


KIKUNDI cha Taarab cha Mashauzi Classic, chini ya uongozi wake Isha Mashauzi, siku ya Idd Mosi kitafanya onyesho la uzinduzi wa albamu yake mpya ya 'Asiyekujua hakuthamini.'

Onyesho hilo litakaloanza saa tatu usiku, limepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Buzuruga Plaza na kiingilio kitakuwa sh. 10,000 kwa mtu mmoja.

Katika onyesho hilo, kutakuwepo  wasanii machachari wenye sauti za kuvutia kama vile Isha Mashauzi (mkurugenzi), Hashim Said,  Thania Msomali, Saida Ramadhani na Zubeidah Andunje

No comments:

Post a Comment