Baada ya baadhi ya mitandao kuandika habari inayohusiana na mafanikio anayoyapata Diamond Platnumz kimuziki baada ya nyimbo yake ya Ntampata Wapi kuchezwa na kituo cha Televisheni cha Ufaransa cha Trace Urban na kufanya vizuri mpaka kufikia kupewa nafasi ya kuchezwa kamaSmash Hit, Diamond alifunguka katika ukurasa wake wa Intagram na kuwashukuru watanzania kwa support wanayompa.
"... Nisingefika hapa bila nguvu na support toka nyumbani... kutoka moyoni kwangu, nawashukuru sana... na aminini kauli yangu, ndio nimeanza... angalieni sinema huu mwaka..." alimalizia Diamond platnumz.
kauli hiyo ilifuatiwa na Comment zaidi ya 450 zikimpongeza na kumsifia.
No comments:
Post a Comment