Shoo hiyo ya Gusagusa Min band na Asia Idarous Khamsin itakayofanyika nchini Uingereza
London, Uingereza
Mbunifu wa mavazi nchini ‘Mama wa Mitindo’, Asia Idarous Khamsin yupo nchini Uingereza akiwa ameambatana na magwiji wa muziki wa taarab kutoka Tanzania, Gusagusa Min Band ambao watafanya maonyesho makubwa ndani ya miji ya nchi hiyo ikiwemo London na Northampton.
Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo nchini humo, Kampuni ya Didas Entertainment ya Uingereza walieleza kuwa, shoo ya kwanza itakuwa Mei 2, katika viunga vya mji wa London na shoo nyingine ni Mei 3 katika mji wa Northampton ambapo kutakuwa na fashion shoo ‘Divas Catwalk’ itakayopambwa na Mama wa Mitindo, Asia Idarous.
Magwji Afua, Mwanahawa, Asya Idarous na Achun Baa meneja wa Gusagusa min Band ndani ya UK.
“Gusagusa Min Band na Mama wa Mitindo, Asia Idarous, Tayari wapo ndani ya viunga vya Uingereza na wapo kamili kwa shoo kabambe Mei 2 ndani ya Empire Suite, London na shoo ya Mei 3, ndani ya Academy, mji wa Northampton. Gusagusa ipo full band nzima ikijumuisha wapiga vyombo wao” ilieleza taarifa hiyo kutoka Didas Entertainment.
Aidha, katika safari hiyo, Asia Idarous ameongozana na wadau wengine wakiwemo Mkurugenzi wa Gusagusa Mind Band, Hasan Farouk, gwiji wa taarab, Bi Afua Suleiman (muimbaji), Bi Mwanahawa Ally (muimbaji), Jaffer bhai (muimbaji), Khamis Chizi (master keyboard ) na Abdulla Ngonda (mpiga base) na wengineo wengi.
Mama wa Mitindo, Asya Idarous Khamsin (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Gusagusa Min Ban, Achun Baa na Hamis chizi 'Master keyboard' ndani ya viunga vya Milton Keynes UK (Uingereza).
Didas Entertainment imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za burudani ikiwemo kupeleka wasanii kutoka Tanzania na kupiga shoo nchini Uingereza pamoja na shughuli zingjne za Sanaa ikiwemo filamu, wasanii wa filamu na uandaaji wa filamu, ambapo hadi mwaka huu imeweza kutimiza miaka 10, tokea kuanzishwa kwake
nice bloh and article, thanks for sharing
ReplyDelete