Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE alizaliwa Oktoba 7, 1950 katika Kijiji cha Msoga, Kata ya Lugoba Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Ni mmoja wa watoto wa Khalfan Kikwete na Asha Binti Jumbe (wote ni marehemu).
Alizaliwa akiitwa Jakaya Khalfan Mrisho Kikwete, na kukua katika familia ya viongozi. Babu yake alikuwa Chifu; baba yake alikuwa kiongozi wa serikali; yeye alianzia katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baba yake mzazi alifariki dunia Agosti 8, 1998, Kinondoni Dar es Salaam; mama yake aliaga dunia Juni mosi, 1999. Mama mzazi wa Rais Kikwete alikuwa ni miongoni mwa wake watano wa Mzee Khalfan aliyekuwa na watoto watatu.
Rais Kikwete ni mwanawe wa pili, akitanguliwa na dada yake mkubwa, Zena (marehemu), na mdogo wake, Mohamed Mrisho Kikwete.
Kabla ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Kikwete alikuwa Waziri kwa miaka 17 ikiwamo miaka 10 ya uwaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aligombea urais katika uchaguzi Mkuu uliopita akashinda, na Desemba 21, 2005 aliapishwa kuwa Rais wa nne wa Tanzania.
Kwa mujibu wa kitabu cha ‘Kikwete, Safari ya Ikulu,’ Rais Kikwete ana watoto saba; wawili kati ya hao, Ridhiwani na Salama alizaa na mke wake wa kwanza, Aziza Sabuni (marehemu); watano amezaa na mkewe wa sasa, Salma ambao ni Miraji, Ally, Khalfan, Mwanaisha na Rashid ‘Chodo’.

No comments:
Post a Comment