SIRI nzito juu ya mauaji ya albino yanayoendelea kutokea sehemu mbalimbali nchini imefichuliwa kufuatia utafiti wa kina uliofanywa na albino wenyewe na sasa wameamua kukifikisha kilio chao kwa Rais Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa utafiti huo, imebainika kuwa watu wanaotumwa kukata viungo hivyo na kuua albino wanapewa fedha nyingi na vigogo ambao huvitumia kishirikina. Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Bw. Ernest Kumaya, wakati akizungumzia maandamano ya amani ya kupinga na kulaani mauaji yanayoendelea dhidi yao nchini. "Tunaamini kabisa watu wanaonunua viungo hivi vya albino ni watu matajiri na wenye madaraka makubwa katika maeneo malimbali ikiwamo serikalini. "Mtu maskini hana uwezo na hawezi kununua kiungo kimoja kinachouzwa sh. milioni 13 hadi 14 ni matajiri ndio wenye uwezo wa kununua," alisisitiza Bw. Kumaya akibainisha waliyoyagundua. Alisema kutokana na hali hiyo wana hofu kubwa katika uchaguzi mkuu wa 2010 viungo vyao vitazidi kuongezeka kwani kipindi hicho cha kuelekea uchaguzi mbalimbali nchini vitendo vya kishirikina pia huongezeka. "Wakati huo kila kiongozi atataka kuhakikisha anashinda, hivyo kwa kuwa viungo vyetu ni biashara, vitendo vya kishirikina vya mauaji ya albino kwa ajili ya kuchukua viungo vyetu vitaendelea kutawala," alisema. Alisema katika uchunguzi wao wa Septemba mwaka huu albino waligundua pia kuwapo kwa kikundi cha watu wasiozidi 10 wakiwamo wanawake ambao wamekuwa wakifanya mauaji hayo. Bw. Kumaya alisema kikundi hicho ambacho kilikuwa kipo Kanda ya Ziwa hasa Mwanza kimehamia Bukoba na baadaye wanahofia kwamba kitahamia Dar es Salaam..
.
Saturday, October 18, 2008
VIGOGO WANAHUSIKA NA MAUAJI YA ALBINO
SIRI nzito juu ya mauaji ya albino yanayoendelea kutokea sehemu mbalimbali nchini imefichuliwa kufuatia utafiti wa kina uliofanywa na albino wenyewe na sasa wameamua kukifikisha kilio chao kwa Rais Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa utafiti huo, imebainika kuwa watu wanaotumwa kukata viungo hivyo na kuua albino wanapewa fedha nyingi na vigogo ambao huvitumia kishirikina. Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Bw. Ernest Kumaya, wakati akizungumzia maandamano ya amani ya kupinga na kulaani mauaji yanayoendelea dhidi yao nchini. "Tunaamini kabisa watu wanaonunua viungo hivi vya albino ni watu matajiri na wenye madaraka makubwa katika maeneo malimbali ikiwamo serikalini. "Mtu maskini hana uwezo na hawezi kununua kiungo kimoja kinachouzwa sh. milioni 13 hadi 14 ni matajiri ndio wenye uwezo wa kununua," alisisitiza Bw. Kumaya akibainisha waliyoyagundua. Alisema kutokana na hali hiyo wana hofu kubwa katika uchaguzi mkuu wa 2010 viungo vyao vitazidi kuongezeka kwani kipindi hicho cha kuelekea uchaguzi mbalimbali nchini vitendo vya kishirikina pia huongezeka. "Wakati huo kila kiongozi atataka kuhakikisha anashinda, hivyo kwa kuwa viungo vyetu ni biashara, vitendo vya kishirikina vya mauaji ya albino kwa ajili ya kuchukua viungo vyetu vitaendelea kutawala," alisema. Alisema katika uchunguzi wao wa Septemba mwaka huu albino waligundua pia kuwapo kwa kikundi cha watu wasiozidi 10 wakiwamo wanawake ambao wamekuwa wakifanya mauaji hayo. Bw. Kumaya alisema kikundi hicho ambacho kilikuwa kipo Kanda ya Ziwa hasa Mwanza kimehamia Bukoba na baadaye wanahofia kwamba kitahamia Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment