.

.

.

.

Thursday, October 02, 2008

HUZUNI MKOANI TABORA

Wafanyakazi wa mochuari ya Tabora leo wakishughulikia maiti za watoto waliopoteza maisha yao kwa kukosa hewa, katika ukumbi wa disko uliopo katika jengo la NSSF .


BREAKING NEWS.......
Simanzi kubwa Tabora, watoto 19
wafariki katika disko la Idd
.Familia mbili zapoteza watoto watano
.Rais Kikwete atuma salamu, atakka uchunguzi wa kina
HUZUNI na simanzi zimetawala kwa wakazi wa mjini Tabora baada ya kupoteza watoto wao 19 katika maafa makubwa yaliyotokea katika ukumbi wa disko wa Bubbles.
Kufuatia tukio hilo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete maelitaka jeshi la polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa kina kufuatia vifo vya watoto hao.

Mbali na kutaka uchungzui huo, pia ametoa pole kwa familia zilizopoteza watoto hao pamoja na wananachi wa mkoa wa Tabora kwa ujumla.

"Nimepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa na niameagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili kujua chanzo halisi cha vifo hivyo na hatua za kisheria zichukjue mkondo wake, "alisema katika taarifa yake ya majonzi kwa famikia zilizopoteza watoto hao.

Askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Galas Okonyo aliyepoteza na watoto wawili aligoma wasizikwe pamoja kama serikali ilivyotaka badala yake anafanya mipango ya kuwapeleka nyumbai kwao Musoma, mkoani Mara.
Maafa hayo yaliyotokea juzi alasiri katika ukumbi huo unaomilikiwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo watoto hao walifariki papo hapo na wengine 60 kuzimia kwa kukosa hewa kabla ya kuokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Akizungumzia juu ya watoto wake, Okonyo alisema alikuwa ametokea safarini mkoani Mara na kwamba aliwasili nyumbani kwake mjini Tabora majira ya saa 11:00 jioni na kumkuta mkewe akamuuliza watoto wameenda wapi.
Alisema mkewe alimjibu kuwa wamekwenda kutembea, lakini wakati wanaendelea kuzungumzia suala hilo, alipokea simu kutoka kwa mtu mmoja aliyemweleza kwamba kuna watoto wamefariki dunia katika ukumbi wa Bubbles baada ya kukosa hewa wakati wanacheza disko kutokana na kujazana.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo na kwa kuwa ukumbi huo hauko mbali na nyumbani kwake, alikwenda na alipofika na kuanza kukagua miili ya watoto waliokufa, mwili wa kwanza kuuona ulikuwa ni wa mtoto wake.
Alisema baada ya kuona hivyo aliamua kumtafuta mwingine na katika kuangalia mwili wa 16 ulikuwa ni wa mtoto wake mwingine.
Aliwataja watoto hao kuwa ni Jacob Galas na Jacob Kasele.
Alisema alikataa watoto wake hao wasizikwe pamoja na wenzao kwa sababu alikuwa ametokea Musoma na babu yao alitaka kuwaona wajukuu wake, hivyo hawezi kukubali wazikwe hapo isipokuwa atawapeleka nyumbani kwao Musoma.
Pia Afisa mmoja wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambaye hakutaka jina lake litajwa gazetini akisema kuwa ana uchungu wa kuondokewa na watoto wake watatu waliofariki katika tukio hilo.
"Jamani naomba niacheni nina uchungu sana moyoni, siwezi kuzungumza sasa hivi, nimepoteza watoto wwatatu, mke wangu pia alifariki Septemba, mwaka huu sasa nimebakia sina mtu, inaniuma sana niache,"alisema mkazi huyo wa Cheyo A mjini hapa.
Afisa huyo wa Takukuru alisema hivi sasa anafanya mipango ya kusafirisha miili ya watoto wake kwenda Songea kwa mazishi.
Jirani wa afisa huyo walisema wamepokea taarifa hizo kwa huzuni sana sababu watoto wa afisa huyo walikuwa wakiishi nao bila matatizo.
Wakati huo huo, wazazi na walezi wameitaka serikali kupiga marufuku madisko kwa watoto na kusimamia sheria kikamilifu na kuwataka wazazi kufuatilia nyendo za watoto wao kikamilifu badala ya kuwaacha huru kupita kiasi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, alisema kuwa amepokea kwa mstuko habari za vifo vya watoto vilivyotokea mjini humo.
"Mimi na familia yangu tunaungana na familia za marehemu kuomboleza vifo hivyo. Hakika mkoa wa Tabora umepatapigo kubwa kwa kuondokewa na vijana hao kwa wakati mmoja vijana ambao walikuwa na ndoto changa za kuchangia kwa njia tofauti maendeleo ya taifa letu," alisema.
Alishauri ufanyike uchunguzi wa kina ili kuepusha matukio ya kuhuzunisha kama hayo kurudia tena
.

No comments:

Post a Comment