.

.

.

.

Wednesday, October 15, 2008

YANGA KUUMANA NA AZAM FC LEO


Makocha wa YANGA katika pozi na mkereketwa wa YANGA Ridhwani Kikwete


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wametamba kuvuna pointi tatu katika mchezo wa leo dhidi ya Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga inaingia uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa na Kagera Sugar mabao 2-0 katika mechi iliyopita ambayo ilichezwa uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera. Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega amesema kuwa, mechi ya leo ni muhimu kwao, hivyo ni lazima waondoke na pointi tatu ili kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri zaidi ya kutwaa ubingwa. "Wachezaji wetu wameandaliwa vizuri na walimu wao hivyo tunaamini kabisa tutaibuka na ushindi katika mechi yetu ya leo," amesema Madega.Amesema macho na masikio ya mashabiki wao yapo kwa timu yao kuona kama itaweza kutafuna mfupa uliomshinda Simba, hivyo ameahidi kuwapa raha mashabiki hao.Wakati, Yanga wakitamba hivyo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Sylvestre Marsh amesema kipigo walichotoa kwa Simba cha mabao 2-0, Yanga nao wategemee hivyo. Marsh amesema kuwa, wamejiandaa vizuri kuikabili timu yoyote watakayocheza nayo bila kuogopa majina ya klabu kongwe. "Wachezaji wetu wamepata uzoefu wa kutosha, mwanzo walikuwa bado ni wageni, lakini sasa wamezoea mikikimikiki ya Ligi Kuu," amesema Marsh.

No comments:

Post a Comment