.

.

.

.

Saturday, November 08, 2008

JUA CALI AFUNIKA LONDON NDANI YA AFRIQUE

Msanii toka Kenya JUA CALI nusura jana usiku avunje rekodi ya wingi wa watu Clubafrique inayoshikiliwa na msanii wa Kitanzania ALI KIBA baada ya kujaza nyomi tele na kuwachengua mashabiki kibao waliohudhuria shoo hiyo ya mwaka.Pamoja na kiingilio kuwa bei ya juu ya £15 kwa kila mtu lakini kila mtu alifurahia jinsi kijana huyo alivyolishambulia jukwaa na kuwapagawisha kina dada waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu na hasa kila alipotaja miji iliyoko nchini kenya na jina la Barack Obama ambaye Tshirt zake ziliuzwa kabla ya onyesho hilo na kuvaliwa na karibu ya nusu ya umati wa watu waliohudhulia.Kwa picha zaidi bofya http://www.tanzaniaone.net/

No comments:

Post a Comment