.

.

.

.

Friday, November 28, 2008

MAAJABU YA TANGA



Maajabu zaidi: Alikuwa mwanaume sasa mwanamke, husherehekea usiku paka wakilia
Tukio hilo ambalo ni la kwanza kutokea mjini hapa, licha ya kustaajabisha wakazi wengi lakini pia inadaiwa kuwatia hofu watu wanaoisikia au kumuona mtoto huyo na hivyo kumfanya kila mmoja kuzungumza lake.Mama mzazi wa mtoto huyo, Rosemary Mhina, alisema kwamba mwanaye alizaliwa Julai 16, 2008 katika Hospitali Teule, Muheza na kwamba mpaka mwezi huu wa Novemba mtoto huyo ameshafanya vituko vinne vinavyomchanganya sana.

Ijumaa: Ni vituko gani hivyo vinavyokushangaza mama Glory?

Rosemary: Kwanza nilipigwa butwaa sana kumsikia mwanangu akilia akiwa tumboni, hilo lilinichanganya na kunifanya niwe na wasiwasi naye.

Ijumaa: Ulichukua hatua gani baada ya kuona hali hiyo?

Rosemary: Niliamua kwenda kupima hospitali ili kujua nina mtoto wa aina gani, ambapo kwa kutumia kipimo cha Ultrasound iligundulika nina mtoto wa kiume.

Ijumaa: Sasa mbona anaonekana wa kike?

Rosemary: Hata mimi nashangaa, ndiyo maana nakwambia ni maajabu.Alielezea kituko cha pili kwamba ni kitendo cha mtoto huyo kutaka kuitwa kwa majina matatu, yaani Glory, Halima na Upendo huku akitoboa siri ya baba yake kumshinikiza mama huyo akaitoe mimba iliyomzaa yeye.Kituko kingine alichokieleza mama huyo ni uwezo wake wa kuwatambua watu wabaya (wachawi) na wema, ingawa imekuwa faraja kwa wakazi wa hapa ambao walimwambia mwandishi wetu kwamba angalau wanaishi kwa amani wakiamini wachawi hawatawasumbua tena.Kituko kikubwa zaidi kinachomshangaza mama wa mtoto huyo ambacho kinamnyima raha ni kuvamiwa na mapaka usiku ambao huwa wanamkwarua lakini cha ajabu mwanaye amekuwa akishangilia.

Rosemary: Ni kama anashangalia wakati mimi naumizwa, yaani nashindwa kabisa kumuelewa huyu mtoto.

Ijumaa: Unafikiri kwanini huwa anashangilia wakati mapaka yakikukwarua?

Rosemary: Kwakweli sijui.

Ijumaa: Umeshafanya jitihada gani hadi sasa juu ya matatizo haya yanayokukabili kuhusu mwanao?

Rosemary: Nilikwenda kwa Walokoke ili wamuombee, lakini pamoja na maombezi hayo, mwanangu hajabadilika na anasumbua sana.

Mama huyo aliomba wasamaria wema ambao wanaweza kujua tiba ya mtoto wake huyo wamsaidie kwani anaishi .

SOURCE: Gazeti la IJUMAA

No comments:

Post a Comment