Watoto wanne wa Kimasai wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu katika kijiji cha Embukoi karibu na eneo la kambi ya mafunzo ya Jeshi la polisi Kilelepori wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro. Wakizungumza jana katika eneo la tukio wananchi wa kijiji hicho wamelaani kitendo kilichotokea kwa madai kuwa wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu katika serikali ya mkoa bila mafanikio. Wamesema kuwa wameshapeleka malalamiko yao Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bwana Mohamed Babu kuhusu madhara yanayowapata. Madhara hayo ni pamoja na mifugo yao kuuwawa pamoja na wanawake wajawazito kuharibika mimba na wazee kupata mishtuko na kufariki dunia kutokana na mabomu na silaha za moto zinazopigwa katika kambi hiyo ambayo iko katika makazi ya watu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Bwana Lucas Ng`hoboko amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewataja watoto hao kuwa ni Larta Lota, Samweli Julius, Liyomomo Olikirima na Rose Saningo na majeruhi ni Isaya Ndiogi ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu. .
.
Wednesday, December 24, 2008
WATOTO WA KIMASAI WAUWAWA KWA MABOMU
Watoto wanne wa Kimasai wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu katika kijiji cha Embukoi karibu na eneo la kambi ya mafunzo ya Jeshi la polisi Kilelepori wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro. Wakizungumza jana katika eneo la tukio wananchi wa kijiji hicho wamelaani kitendo kilichotokea kwa madai kuwa wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu katika serikali ya mkoa bila mafanikio. Wamesema kuwa wameshapeleka malalamiko yao Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bwana Mohamed Babu kuhusu madhara yanayowapata. Madhara hayo ni pamoja na mifugo yao kuuwawa pamoja na wanawake wajawazito kuharibika mimba na wazee kupata mishtuko na kufariki dunia kutokana na mabomu na silaha za moto zinazopigwa katika kambi hiyo ambayo iko katika makazi ya watu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Bwana Lucas Ng`hoboko amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewataja watoto hao kuwa ni Larta Lota, Samweli Julius, Liyomomo Olikirima na Rose Saningo na majeruhi ni Isaya Ndiogi ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment