.

.

.

.

Friday, January 23, 2009

UINGEREZA YAPEWA JOTO NA "EPA"

BALOZI wa Uingereza nchini Tanzania anayemaliza muda wake, Philip Parham amesema suala la EPA liliwaweka katika wakati mgumu kwa sababu walibaini kuwa kumbe fedha za walipa kodi wa Uingereza na wengineo zinatumiwa vibaya.
Akizungumza jana, balozi Parham alisema hiyo ilikuwa ni changamoto kubwa na kulikuwa na hofu kwamba wahisani hasa wale wanaochangia katika bajeti ya Tanzania wangesitisha misaada yao kama serikali isingelichukua hatua madhubuti za kupambana na rushwa na ubadhirifu wa fedha za walipakodi.
Hata hivyo Balozi Parham alisema jitihada zinazochukuliwa na serikali kwa sasa zinatia moyo ingawa hazitoshi, kwani bado kuna mambo mengi zaidi ya kufanya kuhakikisha kwamba kunakuwa na utawala bora na udhibiti mzuri wa matumizi ya fedha za serikali.
Kuhusu rada ya Tanzania iliyonunuliwa Uingereza ambayo inadaiwa kuwa manunuzi yake yalifanyika katika mazingira ya rushwa na serikali ya Tanzania kudai kuwa ikithibitika kama bei ya rada ilikuwa imeongezwa itaiomba Uingereza irudishe fedha iliyozidi, Balozi Parham alisema wanaopaswa kurudisha fedha hizo ni wale waliochukua.

No comments:

Post a Comment