.
.
Wednesday, January 14, 2009
WANAFUNZI 3 WAFA MAJI KIGAMBONI
Wanafunzi watatu wanaosomea udaktari wa binadamu katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Muhimbili wamefariki dunia baada ya kuzama baharini wakati wakiogelea kwenye ufukwe wa kijiji cha Mbwa Maji kule Kigamboni Jijini. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi amesema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 12:25 jioni kwenye ufukwe huo ulioko nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kamanda Kandihabi amesema wanafunzi hao walifika ufukweni kuogolea lakini kwa bahati mbaya maji yakawazidi nguvu na kujikuta wanapoteza maisha. Amesema hadi jana walifanikiwa kupata mwili wa mwanafunzi mmoja aliyefahamika kwa jina la Khatibu Alli Mzee, 23, ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili. Amesema miili ya wanafunzi wengine wawili ambao ni Issa Kennedy, 25, mwanafunzi wa mwaka wa nne na mwenzie, Omari Abdallah, 23, wa mwaka wa pili bado haijapatikana. Kamanda amesema Polisi bado wanaendelea na juhudi za kutafuta miili ya marehemu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment