.

.

.

.

Tuesday, February 24, 2009

KOMAL KATAKIA NAYE AIBUKA MAHAKAMANI ASUBUHI HII


Baada ya kukaa kimya kwa muda baada ya taarifa za utata za kifo cha Komal Katakia, 22, raia wa India ambaye anatuhumiwa kumuua mtu mwingine mwenye asilia ya asia, leo ameibukia mahakamani Kisutu leo yu mzima wa afya.
Komal na mumewe, Vinosh Praven, wanatuhumiwa kumuua mfanyabiashara, Abdulbasiti Abdallah, 21.
Wakati huo huo Mamlaka ya Magereza imetoa ufafanuzi kuwa yule mama wa kihindi aliyedaiwa kufariki duniani akiwa gerezani ama kwa kujinyonga au kuuawa kwa mateso Soma Zaidi kuwa bado yuko hai na ni mzima wa afya. Taarifa hizo zilianza kuzagaa Ijumaa iliyopita na kukolea zaidi Jumamosi namna hii, lakini Msemaji wa Magereza amesema ni uzushi na huyo mama yuu hai.

No comments:

Post a Comment