.

.

.

.

Thursday, March 19, 2009

NGASSA AJA UINGEREZA KUJARIBIWA NA WEST HAM UNITED

TIMU kongwe inayoshiriki Ligi Kuu ya England, West Ham United imempa mwaliko wa majaribio ya wiki mbili, winga wa Yanga na Taifa Stars, Mrisho Ngassa.
Majaribio hayo yamepangwa kuanza Aprili 13 kwa mujibu wa Katibu wa West Ham United, P.R. Barnes.
Barua ya klabu hiyo kwa Yanga kupitia wakala wa FIFA, Bakhressa, Ngassa atagharimiwa kila kitu na timu hiyo wakati wote wa majaribio hayo.
Majaribio hayo yatakuwa chini ya idara ya ufundi ya West Ham inayoongozwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Italia, Giafranco Zola.
Kwa mujibu wa nakala ya barua hiyo, Ngassa anatakiwa kufika England kabla ya tarehe hiyo na maandalizi ya mazoezi hayo yamekwisha kamilika.
Uongozi wa Yanga ulithibitisha kupokea mwaliko na kusema wametoa ruhusa kwa Ngassa kwenda kujiunga na timu hiyo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lucas Kisasa alisema kuwa hawana tatizo na suala hilo kwani wakala wa FIFA aliyekuwepo hapa na klabu hiyo wamefuata utaratibu ambao unakubalika.
“Kumbuka tulimzuia Ngassa kwenda klabu ya Ligi daraja la pili ya Lov Ham ya Norway kutokana na ukiukwaji wa sheria, wakala wa FIFA ametupa taarifa na tumepokea barua ya timu, hapa hakuna jinsi, na nasema tunampa ruhusa kwa ajili ya majaribio,” alisema Kisasa.
“Tayari West Ham wanawasiliana na sisi na wakala wa FIFA, huu ni mwanzo wa uhusiano mpya katika masuala ya kimichezo, tunafarijika sana na tunamwombea Ngassa afanye vyema kama ilivyokuwa kwa Nonda Shaaban,” alisema.

No comments:

Post a Comment