.

.

.

.

Tuesday, March 31, 2009

SIMBA NA YANGA KUUMANA APRIL 26


Mpambano wa Watani wa Jadi unaosubiliwa kwa hamu na wakazi wa Washington Metro area na vitongoji vyake sasa utafanyika siku ya muungano,jumapili april 26 kwenye wanja letu la taifa la zamani(meadowbrook park) na msaidizi Balozi mh. Switebert Mkama kuwa mgeni wa heshima.
Mara ya mwisho timu hizi ziliumana vikali June 15 mwaka jana na vijana hao wa msimbazi walisalimu amri ya bao 4-1 dhidi ya mahasimu wao Yanga ambao mwaka huu imezidi kuimarika baada ya kusajili vijana wapya,japo uongozi wa Yanga ulikataa kutaja majina ya usajili huo.kwa upande wa Simba Mkakile(Bamchawi) yeye ametamba kwamaba mwaka huu ni mwaka wao uteja kwa Yanga basi na habari tulizo zipokea hizi punde kutoka ndani ya uongozi wa Simba,kamati ya ufundi imepata mtaalamu kutoka Bwagamoyo ambae watamjaribu kwenye mpambano huo ambo unategemewa kuwa mkali na wenye vitmbi vingi.
Simba wamepata uzi mpya kutoka kwa mfadhili ambae hakutaka jina lake litajwe,jezi hizo zimeipa kiwewe Uongozi wa Yanga unaohangaika kushinda kwa wafadhili kujaribu nao wapate Jezi.Sisi hata kama tutakosa jezi,kuifunga Simba ni kama kumsukuma mlevi,sisi tutarudia kile kipigo june 15,Simba wao wana sema Yanga kuongea jadi yao mwaka huu mkichungulia tu ni kipigo cha mbwa mwizi.mbali na mpambano huo,kutakuepo na nyama choma na kikombe kwa mshindi

Wakati huo huo timu ya Bongo United Fc,inayo jiandaa na mpambano na Houston Stars may 24,ipo kwenye mazoezi makali chini supa kochi Gharib Latto na mpaka sasa imeisha cheza mechi 4 za kujipima nguvu,Senegal,Malawi,Togo na Nigeria na imeshinda mechi 3 na kutoka droo na Nigeria,na April 11 itaelekea Nc kwa mpambano wa kirafiki.Ujumbe kwa Houston,Nyama ikishaingia Buchani Hairudi kua ng'ombe Ole wenu Houstoni Mkichungulia tu Hamtoki.

No comments:

Post a Comment