WAFANYAKAZI wanaokadiriwa kufikia 150 kati ya 297 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), watapunguzwa kazi ili kuweka uwiano kati ya watumishi na idadi ya ndege zinazotoa huduma ndani ya shirika hilo, Mwananchi imebaini.
Kwa muda mrefu, ATCL imekuwa ikishutumiwa kwa kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi isiyolingana na ndege inazomiliki. Habari za kuaminika zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa wafanyakazi hao wanatakiwa wawe wamepunguzwa kazi ifikapo Mei, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mikakati inayofanyika sasa ni mchakato wa kuandaa hesabu za mafao ya wafanyakazi hao, zoezi linalofanywa kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha na Uchumi.
Shirika hilo la umma ambalo lipo kwenye harakati ya kuendeshwa kwa ubia kati ya serikali na kampuni moja ya China, kwa sasa lina ndege mbili tu ambazo zinatoa huduma ya usafiri ndani ya nchi.
Katika idadi hiyo ya wafanyakazi 150 watakaopunguzwa, wachache ambao ATCL itawahitaji baada ya kuongeza idadi ya ndege zake, watapewa likizo ya bila malipo kwa muda usiojulikana.
Miongoni mwa waliomo kwenye orodha ya kupewa likizo bila malipo wamo marubani na watendaji wa ndege, ambao ni adimu katika sekta ya usafiri wa anga.
ATCL kwa sasa ina marubani wazalendo 20 na wengi kati ya hao wakiwa katika orodha ya kupewa likizo hiyo bila malipo. Hata hivyo, suala la kupewa likizo bila malipo limekuwa na mvutano mkali kiasi cha kusababisha mpango wa kufanikisha zoezi hilo kusuasua.
Inaelezwa kuwa hali hiyo inatokana na Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (COTWU), kuweka wazi kuwa hakuna sheria inayoruhusu mfanyakazi kupewa likizo ya bila malipo.
Chanzo chetu kinapasha kuwa mazingira hayo yanaashiria kuwa huenda wafanyakazi hao adimu wakawekwa katika orodha ya watakaopunguzwa, lakini baadaye wataajiriwa upya kutokana na umuhimu wao.

No comments:
Post a Comment