.

.

.

.

Tuesday, April 28, 2009

KHANGA NA VITENGE


Vivazi vilivyoundwa kwa kutumia vitambaa vya vitenge na Kanga vimechukua nafasi kubwa katika anga la mitindo si Bongo pekee kwani hata nchi za wenzetu tumeshuhudia hilo.Madezigner wengi wa hao wa nyumbani wamejikita katika matumizi ya kanga na kama hawatotumia kwa vazi lolote, basi vazi litanakshiwa kwa kanga au kitenge.Nimeweza kushuhudia kwa wabunifu kama Mustafa Hassanali,Asia Idarus,Khadija Mwanamboka, Robby , Fatma Amour na wengineo wengi.Nilimshuhudia pia mwanamuziki wa Marekani Estella akiwa wametinga vazi lililoshonwa kwa Kanga, hakika inavutia.Siku za karibuni wabunifu watanzania kupitia mitindo House walifnya onesho la mavazi nakulipa jina la Kimaso maso ambapo walikuwa na nia ya kuonyesha mavazi ya maharusi wenye asili ya kiafrika mwisho wasiku walijikuta wengi wakiwa wametumia kanga na vitenge kama nakshi ya mavazo hayo.Habari ndo iyooo kama nawe ni mteja wa Fashion jitahidi uwe na kamshono ka kanga kama si kitenge shost.
No comments:

Post a Comment