Shindano la MAISHA PLUS ambalo limekuwa kivutio kikubwa kwa watazamaji wa kituo cha televisheni ya Taifa TBC1 na ambalo limeanza kuteka na kuvuta hisia za mashabiki karibu Tanzania Nzima linatarajia kuanza Tena hivi karibu, akizungumzia Shindano mkurugenzi wa Maisha Masoud kipanya amesema Usaili umenza jana tarehe 22 Julai kwa kugawa fomu maeneo mablimbali kwa kuzingatia mgawanyo wa kikanda,Vilevile Mshindi wa maisha plus wa shindano lililopita Abdull ambaye alitokea Zanzibar alisema shindano la maisha Plus ni zaidi ya Maisha kwani unajifunza vitu vingi ikiwemo mbinu ya kuishi na watu mbalimbali wenye tabia tofauti vilevile unapata maisha halisi ya Kijijini na Uhalisia wake.
Mkurugenzi huyo wa MAISHA PLUS Masoud Kipanya ameongeza na kueleza kwa upana maana ya kipindi hicho kuwa ni kuelezea jamii kwa upana wake uhalisia wa kipindi hicho na uelewa wa kutafakari mambo kwa upana zaidi na kujifunza mambo Mengi zaidi kimaisha hasa maisha ya mtanzania wa kawaida anayeishi kijijini.Zawadi ya Msimu huu ni shilingi Milioni 15 Vigezo vya Msingi vya kuweza Kushiriki ni Umri kati ya miaka ishirini na moja na ishirini na sita Elimu ya Sekondari au iliyo sawa na sekondari au chuo cha ufundi na awe na Uraia wa Tanzania, vijana wote wana ruhusiwa kushiriki waliooa na kuolewa na wasiooa na wasioolewa, ili kujua fomu za kujiunga kwenye usaili zinapatikana wapi angalia tangazo kwenye kituo cha televisheni ya Taifa TBC1.
No comments:
Post a Comment