.

.

.

.

Saturday, July 18, 2009

RAIS YOWERI KAGUTA M7




MIAKA 23 baada ya kuwa madarakani, Rais Yoweri Museveni anasema kwamba bado ana nguvu kuendelea kuwa kiongozi wa Uganda kwa miaka mingine 10.
Museveni, ambaye kwa ajili yake Bunge liliondoa kikomo vipindi viwili vya Urais katika katiba kumruuhsu asimamae tena kiugombea Urais katika Uchaguzi wa mwaka 2006, anasema hana mpango kwa kufanya marekebisho mengine ya kuzidisha umri wa miaka 75 uliowekwa.
Museveni, ambaye atafikisha umri wa miaka 65 Septemba, aliulizwa katika kipindi cha mazungumzo cha usiku cha televisheni mwishoni mwa wiki kama ataendelea kugombea Urais hadi atakapofikisha umri wa miaka 75.
"Lakini ukiwa na umri wa miaka 75 katiba inakuruhusu kugombea," alisema rais huyo. Alipobanwa zaidi aeleze kama atafanya kampeni ya kuondoa kikomo cha umri kama alivvyofanya kuondoa ukomo wa vipindi Museveni alisema: "Hapana; hilo siwezi kuliruhusu."
Rais Museveni amekwua madarakani kwa muda mrefu kuliko marais wote wa zamani waliowahi kuliongoza taifa hilo tokea uhuru mwaka 1962 wawwekwee pamoja.
Aliukwaa Urais mwaka 1986 na kusimama katika chaguzi za miaka 1996, 2001 na 2006.
Wakati mashabiki wake wanasema ameifanya nchi hiyo iwe imara baada ya kuwa na misukosuko ya kisiasa kwa muda mrefu na amesimamia ipasavyo kukua kwa uchumi, wanaompinga wanasema kukataa kwake kukubali mabadiliko ya uongozi kwa njia ya kura ni hatari kwa suala la kuimarika na maendeleo ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment